Nchini Rwanda picha za video zinazoonesha tukio la kushangaza la kimbunga cha majini zimeibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii nchini Rwanda.
Tukio hilo la ajabu la hali ya hewa lilitokea katika ziwa Ruhondo kaskazini mwa Rwanda Jumanne.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini Rwanda inasema kimbunga hicho cha majini husababishwa na upepo mkali unaopaa mawinguni kutokana na utofauti mkubwa wa joto lililopo ziwani na joto la wingu, na mara nyingi wingu hilo husababisha mvua na radi , tukio ambalo huitwa ‘’cumulonimbus’’ kwa lugha ya kitaalamu.
Kimbunga hiki huwa na kasi ya kati ya mita 5 na 8 kwa sekunde na kinaweza kudumu kwa muda wa hadi dakika 20’’, Imesema taarifa ya Mamlaka ya hali ya hewa.
Katika mtandao wa kijamii wa Twitter watu wamekuwa washirikishana picha na video za tukio hilo.

No comments:
Post a Comment