Search This Blog

Saturday, April 17, 2021

Kikosi cha usalama cha Urusi kinamshikilia mwanadipolomasia wa Ukraine


Shirika la upelelezi la Urusi - FSB linamshikilia mwanadiplomasia wa Ukraine, Oleksandr Sosoniuk huko St Petersburg. 

Habari hizo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax, likinukuu idara hiyo ikizungumza leo.Shirika hilo limenukuu FSB ikieleza Sosoniuk alijaribu kujinyakulia nyaraka muhimu katika mfumo wa uhifadhi wa data za utekelezaji wa sheria wa Urusi.

Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza Reuters, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine haikuweza kupatikana mara moja kwa ajili ya kuthibitisha taarifa hiyo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...