Na Timothy Itembe Mara.
KANISA la Romani Katoliki parokia ya mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo wilayani Tarime limekabidhi jengo la vyumba 19 kwa wananchi wa kijiji cha Kewamamba kwa lengo la kujenga mahusiano mema na kuunga juhudi za serikali katika kutekeleza shuguli za maendeleo.
Akikabidhiwa jengo hilo mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri kwaniaba ya wananchi wa kijiji cha Kewamamba na Paroko Lukas Chacha alisema kukabidhi jengo hilo ni moja ya juhudi za kuunga Serikali katika kutekeleza shuguli za maendeleo kwa wananchi wake.
Chacha aliongeza kusema lengo la kukabidhi jengo hilo kwa wananchi wa halmashauri ya Tarime wanamategemeo kuwa jengo hilo litaenda kubadilishiwa matumizi na kuwa moja ya Zahanati ili kuondoa uhaba uliopo kwa wananchi hao wa zahanati,vituo vya Afya pamoja na Hospitali katika jamii ya Tarime.
Chacha aliongeza kusema jengo hilo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 128,852,000 fedha ambazo nimichangom kutoka kwa waumini wa kanisa hilo pamoja na wadau mbalimbali wanaoguswa na shuguli za maendeleo kwa wananchi wa wilaya Tarime na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri alipongeza kanisa hilo na kuomba taasisi mbalimbali pamoja na wale ambao wanaguswa kujitokeza katika kuunga serikali katika kutekeleza shuguli za maendeleo kwa watanzania ili kuwaondolea changamoto zilizopo.
Msafiri aliongeza kusema kuwa Wananchi pamoja na halmashauri waendelee kulinda miundombimu yake huku wakitumia jengo hilo kwa matumizi ya makusudi yaliyokusudiwa na kanisa hilo huku wakijua kuwa kanisa limejinyima na kutumia fedha zao na kujenga jengo na kukabidhi kwao.
Naye Rhobi John Diwani kata ya Kyore alishukuru kanisa hilo na kusema kuwepo kwa Zahanati katika kijiji hicho kutasaidia kuwaondolewa wananchi wake ambao walikuwa wakitembea mwendo mrefu wakifuata huduma katika hospitali ya wilaya ambayo inamilikiwa na halmashauri ya Mji wa Tarime taklibani kilomita zaidi ya 40 kwenda na kurudi.
Kwa upande wa mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime,Apoll Tindwa alichukua hatua ya kushukuru na kupongeza kanisa la Romani Katoliki na kuomba wadau pamoja na wale wote wanaoguswa na maendeleo kujitokeza ka kuunga juhudi za maendeleo kuliko kuendelea kulalamika vijiweni.

No comments:
Post a Comment