Japan inaendeleza mchakato wa kutoa chanjo kwa umma. Katika mchakato mpya, chanjo ya corona (Covid-19) itaanza kutolewa kwa watu walio na umri wa miaka 65 na zaidi.
Wizara ya Afya, Kazi na Ustawi ya Japan, imeanzisha mchakato wa chanjo kwa watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi, ambao ni asilimia 30 ya idadi ya watu wote nchini.
Shirika la Kyodo liliripoti kuwa katika majimbo 39 kati ya 47 ya Japan, watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi walipewa chanjo katika vituo vya kliniki, taasisi za jamii na kumbi za mazoezi.
Kulingana na data ya Wizara, hadi kufikia Ijumaa Aprili 9, dozi milioni 1.1 za kwanza za chanjo ziliweza kutolewa kwa wafanyakazi wa huduma ya afya kote nchini.
Japana inalenga kuwapa chanjo wafanyikazi wa huduma ya afya milioni 4.8 kufikia wiki ya tatu ya mwezi Mei.
Serikali ilitangaza kwamba jumla ya dozi milioni 314 za chanjo ziliagizwa kutoka kwa kampuni za BioNTech-Pfizer, AstraZeneca na Moderna.

No comments:
Post a Comment