Kiwanda cha nyuklia nchini Iran kilipigwa na "hujuma " siku moja baada ya kufichua kifaa kipya cha urutubishaji wa madini ya urani, amesema afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya nyuklia nchini Iran.
Ali Akbar Salehi hakusema ni nani wa kulaumiwa kwa "kitendo cha ugaidi ", kilichosababisha kukatika kwa umeme katika kituo cha nyuklia cha Natanz kilichopo kusini mwa mji wa Tehran siku ya Jumapili.
Vyombo vya habari vya umma vya Israel, hatahivyo, vilinukuu vyanzo vya ujasusi ambavyo vilisema yalikuwa ni matokeo ya mashambulio ya kimtandao ya Israeli.
Israel bado haijatoa kauli yoyote ya moja kwa moja kuhusiana na tukio hilo.
Lakini katika siku za hivi karibuni imekuwa ikichukua tahadhari za mara kwa mara kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Tukio la hivi karibuni linakuja huku juhudi za kidiplomasia za kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 - uliotelekezwa na Marekani chini ya utawala wa Trump katika mwaka 2018 - zikiwa zimefufuliwa.
Jumamosi, rais wa Iran Hassan Rouhani alizindua matumizi ya vifaa vya kutengeneza nyuklia katika eneo la Natanz katika sherehe ambazo zilitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa.
Vifaa hivyo vinavyofahamika kama Centrifuges vilihitajika kuzalisha urani, ambayo inaweza kutumika kutengeneza mafuta ya vilipuzi pamoja na silaha za nyuklia.
Uzinduzi wa vijfaa hivyo pia ulionesha uvunjaji mwingine wa nchi hiyo wa mkataba iliousaini wa mwaka 2015, ambao unairuhusu Iran kuzalisha na kutunza kiwango kidogo cha uruniam iliyorutubishwa kwa ajili ya kutengeneza mafuta kwa ajili nishati ya viwanda vya kibiashara pekee.
Jumapili, msemaji wa Shirika udhibiti wa ishati ya Atomic nchini Iran (AEOI), Behrouz Kamalvandi, alisema "tukio" lilitokea asubuhi likihusisha mtandao wa nishati wa kituo hicho.
Bw Kamalvandi hakutoa maelezo zaidi lakini aliliambia shirika la habari la Iran -Fars kwamba "hapakuwa na majeruhi wala uvujaji ".
Baadae taarifa ya televisheni ya taifa iliyotolewa na mkuu wa AEOI Ali Akbar Salehi, elezea tukio hilo kama "hujuma" na "ugaidi wa nyuklia''.
"Ikilaani hatua hatua mbaya ya shambulio hilo , Jamuhuri ya kiislamu ya Iran ilisisitiza juu ya haja ya jamii ya kimtaifa Shirika la kimataifa la udhibiti wa nguvu za Atomiki [IAEA] kushugulikia ugaidi huu wa kinyuklia ," alinukuliwa akisema.
"Iran ina haki ya kuchukua hatua dhidi ya wahusika," aliongeza.
IAEA ilisema kuwa inatambua kuhusu taarifa za tukio lakini haikutoa kauli.
Mwezi Julai mwaka jana, pia hujuma zililaumiwa kwa moto uliowaka kwenye kiwanda cha nyuklia cha Natanz, ambako shughuli za kifaa cha centrifuge kilipigwa zinaendeshwa.

No comments:
Post a Comment