Search This Blog

Saturday, April 10, 2021

IGP Sirro apata pigo, afiwa na mama yake mzazi


Mama mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Nyakoro Sirro, Bi. Monica Tongori Nyabyamari amefariki dunia usiku wa kuamkia leo April 10 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP, David Misime, msiba upo nyumbani kwa IGP Sirro, Masaki Dar es Salaam, karibu na nyumbani kwa Hayati Benjamin W. Mkapa.

Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu katika Kijiji cha Kiabakari, Wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...