Search This Blog

Thursday, April 15, 2021

Harry Kane aomba kuondoka Tottenham

 


HARRY Kane, mshambuliaji wa Tottenham anataka kuomba kuondoka kwenye kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu.

Nyota huyo raia wa England amekuwa kwenye kiwango bora muda mwingi ila hana bahati ya kutwaa mataji ndani ya kikosi hicho.

Kane amesema kuwa anahitaji kuomba kuondoka kwenye kikosi hicho msimu huu ili akapate changaoto mpya.

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo anataka kwenda kuwatumia Real Madrid ama PSG licha ya kwamba yeye mwenyewe hajaweka wazi suala hilo.

Nyota huyo mwenye miaka 27 mkataba wake na Tottenham unatarajiwa kumalizika mwaka 2024 kwa kuwa alisaini mkataba wa miaka sita 2018. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...