Search This Blog

Sunday, April 11, 2021

Guelleh ashinda muhula wa tano wa urais Djibouti

 


Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh ameshinda muhula wa tano madarakani katika uchaguzi mkuu uliosusiwa na wapinzani wengi. 


Takwimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani zimeonesha kuwa Guelleh ameshinda uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 97 ya kura zilizopigwa, huku mgombea wa upinzani, Zakaria Ismail Farah, akiwa na asilimia 2.48. 


Hata hivyo, Farah amedai kuwa matokeo hayo hayalingani na uhalisia, akisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu. Mshauri mkuu wa Rais Guelleh, Alexis Mohamed, amekanusha madai ya kuwepo udanganyifu, akisema mwenyewe Farah alisusia kupiga kura. 


Akizungumza na shirika la habari la Reuters, kiongozi huyo wa upinzani alisema hakupiga kura kwa kuwa amekuwa akikandamizwa na vyombo vya dola tangu mwanzo wa kampeni hadi kwenye uchaguzi wenyewe. Viongozi wa Ethiopia na Somalia wamempongeza Guelleh kwa ushindi huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...