Search This Blog

Monday, April 26, 2021

Dk.Mpango aweka wazi matumzi ya fedha za Muungano

 


Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amesema fedha ambazo zilikuwa zitumike kwaajili ya kuadhimisha sikukuu ya muungano zimegawanywa katika pande zote mbili kwaajili ya miradi ya maendeleo.

Dk Mpango ameyasema hayo leo Jumatatu Aprili 25, kwenye kongamano la Muungano linalofanyika jijini Dodoma.

Amesema kwa busara za Rais Samia Suluhu amefanya uwamuzi mwaka huu kuadhimisha sikuu ya muungano kwa kufanya kongamano na fedha ambazo zilikuwa zitumike zigawanywe kwenye pande zote mbili za muungano na kila upande utaamua namna ya kuzitumia kwaajili ya shughuli za maendeleo.

"Kwa busara ya mamayetu baada ya kufanya uwamuzi kwamba mwaka huu tuadhimishe muungano wetu kwa kufanya kongamano ameagiza fedha ambazo zilikuwa zitumike kwaajili ya sherehe mwaka huu zitagawanywa kwenda pande zote mbili za muungano na kila upande utaamua namna ya kutumia hizo fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo," amesema Dk Mpango



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...