DJ Khaled ameripotiwa kuliuza jumba lake la kifahari lililopo huko Beverly Hills Marekani kwa kiasi cha $12.5 millioni ambazo ni takribani Sh. Bilioni 30 za Kitanzania.
Kwa mujibu wa ripoti, #DJKhaled ameuza jumba hilo kwa faida kwani mwaka 2016 alilinunua kwa kiasi cha $9.9 millioni ambazo ni takribani Bilioni 23 kwa thamani ya pesa ya Tanzania.
Jumba hilo linatajwa kununuliwa na daktari wa upasuaji David Amron na mkewe Jessica, likiwa na ekari 3 na robo, vyumba 6 vya kulala, mabafu 8, jiko kubwa, gym na mengine mengi ya kuvutia.

No comments:
Post a Comment