China imeishambulia Marekani na Japan kwa kuonesha umoja wao wakati wa mazungumzo kati ya Rais Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga, ikikiita kitendo hicho kuwa ni dhihaka ya jaribio la kuchochea mgawanyiko.
China imesema mkutano wa waandishi wa habari wa Suga na Biden jana Ijumaa, ambao pia walitoa taarifa ya pamoja kuhusu demokrasia na haki za binaadam na kuonesha wasiwasi wao kuhusu vitendo vya China katika ukanda wa Indo-Pacific, ulikwenda nje ya mipaka ya mahusiano yao ya kawaida ya maendeleo.
Katika taarifa yake, ubalozi wa China mjini Washington umesema sio jambo la mzaha kwa jaribio hilo la ujenzi wa kambi dhidi ya mataifa mengine na kwa kitumia kigezo cha uhuru na uwazi.
Katika taarifa ya pamoja ya Japan na Marekani, viongozi hao pia waligusia umuhimu wa amani na utulivu katika ujia wa Taiwan, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa Japan kuzungumzia katika mazungumzo na Marekani juu ya Taiwan tangu mazungumzo ya 1969 kati ya Richard Nixon na Eisaku Sato.

No comments:
Post a Comment