Na Omary Mngindo, Kibaha
CHAMA Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani kinawakaribisha Wawekezaji wataoweza kujenga uwanja wa kisasa wa Mpira wa Miguu uliopo eneo la Mkuza Kata ya Mkuza Halmashauri ya Mji mkoani hapa.
Hatua hiyo inalenga kuongeza fursa ya mapato katika Halmashauri hiyo, inayopigabia kuoanda hadhi ya kuwa Manispaa kutoka Mji, ambapo uwepo wa uwanja utaongeza hamasa ya michezo kwa wana-Kibaha.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa chama hicho Ramadhani Maneno baada ya kuibuliwa kwa hoja hiyo kutoka kwa Diwani Karimu Mtambo, aliyehoji malengo ya chama hicho kwenye eneo hilo ambalo liliwahi kuwekwa jiwe la msingi na Rais wa awamu ya kwabza Hayari Julius Kambarage Nyerere.
"Hili la uwanja pamoja na kwamba linamilikiwa na chama, lakini chama ni wananchi hivyo niwaombe kuanzia sasa tupo tayari kumpokea mwekezaji yeyote atayekuwa tayari kuja kuujenga uwanja wetu ili nasi tuwe na uwanja wenye hadhi utaondelea kuubea mkoa wetu," alisema Maneno.
Awali Mtambo alisema kuwa uwanja huo uliokuwa tegemeo katika kipindi hicho kulipowekwa jiwe la msibgi, ambapo ujenzi wake ulikuwa wachezaji waingie uwanjani wakitokea kama sehemu ya kwenye shimo, kwa maana uwanja ulikuwa uwe kwa juu.
Akichangia mada katika hilo Mkurugenzi Mtendaji Kibaha Mji Jenipha Omilo alisema kuwa katika eneo hilo ambalo lina viwanja viwili, kimoja wapo ambacho kimeshazungushiwa uzio nao kama halmashauri aaliwekeza kiasi cha pesa ikiwa kuuunga mkono uwanja utumike lakini imeshindikana.
"Uwanja huo ukijengwa utasaidia juhudi za Halmashauri kuiona Mmanispaa inakamilika, nikuombe Mwenyekiti hili utusaidie," alimalizia Omolo.

No comments:
Post a Comment