Search This Blog

Friday, April 23, 2021

Canada yazuia ndege zote kutoka India na Pakistan

 


Canada imezizuia ndege zote zinazotoka India na Pakistan kwa siku 30 kutokana na ongezeko la maambukizi ya COVID-19 katika ukanda huo. 

Marufuku hiyo imeanza kutekelezwa jana jioni, ikiwa ni saa chache baada ya India kuripoti maambukizi mapya zaidi ya laki tatu katika saa 24 zilizopita. 

Wizara ya afya ya Canada imesema nusu ya watu walioambukizwa COVID wanaowasili kwa ndege wanatokea India na idadi kubwa pia kutoka Pakistan. 

Umoja wa Falme za Kiarabu nao pia umezuia ndege zote kutoka India kutokana na wasiwasi huo. New Delhi imetoa onyo kwamba wagonjwa wanaweza kufa ikiwa vifaa vya oksijeni katika hospitali havitaongezwa. 

Mfumo wa afya nchini humo unatajwa kuzidiwa na wimbi la pili lililochangiwa na aina mpya ya virusi vinavyoenea kwa kasi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...