Na Ahmad Mmow, Kilwa.
Aliyepata kuwa mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Seleman Bungara(Bwege) amesema utendaji na kauli za Rais Samia zinatia matumaini na anamuunga mkono.
Bwege ameyasema hayo leo mjini Kilwa Masoko alipozungumza na Muungwana Blog baada ya kuombwa aeleze maoni yake dhidi ya utawala wa awamu ya sita.
Bwege ambae alikuwa ni miongoni mwa wabunge machachari ndani bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema anaunga mkono na kufurahishwa na utendaji na kauli za Rais Samia. Kwani zinaleta matumaini katika mshikamano, umoja wa kitaifa, ukuaji uchumi na umairishaji demokrasia.
Alisema kitendo cha Rais Samia kuahidi kuendelea kutekeleza miradi mikubwa na yakimkakati nijambo jema ambalo linastahili kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo.
Kuhusu demokrasia, kada huyo wa chama cha Allience for Change and Transparency(ACT-Wazalendo) alisema kauli za Rais Samia zinaleta matumaini makubwa kwamba demokrasia itaheshimiwa na kwamba itakuwa inanafasi.
Alibainisha kwamba kwamuda mrefu kilichokuwa kinakosekana ni kuheshimu katiba ya nchi na kuruhusu demokrasia ichukue mkondo wake.
Mambo ambayo Rais Samia anaonekana kuruhusu katika kipindi chake cha uongozi wa nchi.
Alisema kitendo cha Rais kuahidi atazingatia utawala wa sheria na ilani ya CCM ni ushahidi kwamba ameamua kuimarisha umoja na mshikamano.
Kwani kusimamia sheria nikuheshimu katiba ya nchi, na kutekeleza ilani ya uchaguzi ni kusimamia na kuimarisha demokrasia. Kwani ilani ya CCM inahimiza umoja, mshikamano, upendo na kuheshimu demokrasia.
'' Mbali nakushinda uchaguzi lakini atakuwa mshindi katika historia, itamkumbuka iwapo atasimamia kikamilifu anayoahidi. Kwani nasisi tuliyokuwa tunataka yafanyike ni hayo.
Asimamie misingi 17 ya demokrasia,''alisema Bwege.
Bwege alikwenda mbali kwakusema '' Kwa mwendo anaokwenda atakuwa ametunyima ajenda mwaka 2025, hasa kuhusu yeye. Kama atagombea atakuwa amejitengenezea mazingira ya yeye kushinda kirahisi bila kutumia maguvu na vitisho,''.
Alitabiri kwamba utendaji wa Rais Samia unatoa sura kwamba kuna uwezekano mkubwa wa wagombea ubunge na udiwani wa vyama vya upinzani kushinda katika uchaguzi ujao.
Lakini nafasi ya Urais itachukuliwa na Samia iwapo atataka kugombea.
Bwege alifafanua kwamba uwezekano wa wagombea wa vyama upinzani kushinda utatokana na uwezo nakukubalika kwa wagombea na nguvu za chama katika kata na majimbo husika.
Alitoa wito kwakila mpenda maendeleo kuunga mkono jitihada za Rais.
Huku akihimiza kwamba uwepo ukosoaji wenye tija kwa nchi na kutoa mapendekezo na ushauri wenye tija.

No comments:
Post a Comment