Umoja wa Afrika(AU) umesitisha mpango wa kupata chanjo ya corona kutoka taasisi ya Serum kutoka India kwasababu ya kuhofia usambazaji wake na badala yake imeamua kuagiza kwa watengenezaji wa dawa wa Marekani, Johnson & Johnson.
Kiongozi wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika,John Nkengasong, alisema ni muhimu kuwa na upatikanaji wa chanjo wa kuaminika - na marufuku ya usafirishaji iliyoko India inaleta changamoto kwa Afrika.
Aliongeza kusema kuwa maamuzi ya Umoja wa Afrika ya kusitisha uagizaji wa Astrazenica hayana uhusiano wowote na athari za watu kuganda damu kutokana na chanjo ya Oxford-AstraZeneca ambazo zitaendelea kuletwa Afrika kutoka Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa Covax.
Taasisi ya India ya Serum ina leseni ya kusambaza dawa ya AstraZeneca duniani kote lakini Delhi imeweka udhibiti ili kukabiliana na maambukizi makubwa.
Bwana Nkengasong alisema AU tayari imesaini mkataba wa milioni 400 ya dozi za Johnson & Johnson.

No comments:
Post a Comment