Search This Blog

Thursday, April 29, 2021

Askari wanne watimuliwa kazi, wengine wasimamishwa wakituhumiwa kupokea rushwa ya Sh100 milioni


 Askari wanne wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamefukuzwa kazi  na  maofisa wawili wa jeshi hilo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh100 milioni.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi Aprili 29 ,2021 na kubainisha kuwa walipokea taarifa kuhusu askari hao Aprili 19, 2021 kwamba wameomba na kupokea rushwa na uchunguzi ukaanza.

"Baada ya uchunguzi jeshi limewafukuza kazi askari wanne na kuwasimamisha kazi  maofisa wawili kwa kuwa haliwezi kuvumilia tuhuma hizi,” amesema.

Amebainisha kuwa baada ya uamuzi huo hatua nyingine za kisheria zinafanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Askari hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa Profesa Justine Maeda ambaye amewahi kuwa mshauri wa uchumi wa rais wa awamu ya kwanza, Hayati  Julius Nyerere.

Wanadaiwa kuomba fedha hizo na kupatiwa baada ya kumpekua nyumbani kwake na kudai kukuta  vipande viwili vya meno ya tembo vikiwa kwenye mzinga wa nyuki.

Profesa Maeda ameieleza Mwananchi Digital kuwa alitoa fedha hizo ili ajinusuru asifunguliwe kesi ya uhujumu uchumi kama alivyoelezwa na polisi hao.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...