Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

8 wafariki wengine zaidi ya 100 wajeruhiwa kwenye ajali ya treni ya abiria iliyotokea nchini Misri


Watu 8 walifariki na wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa kwenye ajali ya treni ya abiria iliyotokea huko Kalyubiye nchini Misri.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Reli ya Misri, treni ya abiria ya Cairo-Mansura ya namba 949, ilikuwa ikisafiri kutoka jiji la Kalyubiye ambapo mabehewa 4 yalipinduka baada ya kutoka nje ya reli.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa afisa ambaye hakutaja jina lake, watu 8 walifariki na wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa.

Idadi kubwa ya magari ya wagonjwa yalipelekwa katika eneo la tukio.

Ajali nyingine ya treni pia iliwahi kutokea Misri mnamo Machi 26, ambapo watu 32 walifariki na wengine 66 walijeruhiwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...