Wapiganaji wanaosadikiwa kuwa ni wanamgambo wa ADF wamewauwa watu wasiopungua 12 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msimamizi wa Mkoa wa Beni Donat Kibuana ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mauaji hayo ya wakulima waliokuwa kwenye mashamba yao yametokea katika kijiji cha Mabule.
Wanaume wanane na wanawake wanne ni miongoni mwa watu waliouawa kwa kukatwa shingo. Kibuana amesema kuwa hata hivyo operesheni za kijeshi katika eneo la mlima Rwenzori mapema mwezi Januari, zimesaidia kupunguza mashambulio katika eneo hilo.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosimia maswala ya haki za binadamu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepongeza juhudi za vikosi vya usalama katika kupambana na makundi ya wanamgambo.

No comments:
Post a Comment