Baraza la Seneti nchini Marekani limemuidhinisha Gavana wa zamani wa Michigan Jennifer Granholm, aliyeteuliwa na Rais Joe Biden kuhudumu katika Wizara ya Nishati.
Katika mchakato wa upigaji kura wa Baraza la Seneti, maseneta 64 walipiga kura ya "ndio" kuunga mkono uteuzi huo dhidi ya maseneta 35 waliopiga kura ya "hapana" kumpinga Granholm kuwa Waziri wa Nishati.
Jennifer Granholm aliwahi kuwa Gavana wa Michigan kuanzia mwaka 2003 hadi 2011.
Granholm anatarajiwa kufanya kazi ili kuhakikisha mpito wa nishati safi kwa kuzingatia lengo la Biden la kuifanya nchi kuwa na kiwango kidogo cha kaboni ifikapo mwaka 2050.

No comments:
Post a Comment