Search This Blog

Wednesday, February 24, 2021

Waziri Kaleman ametoa siku kumi kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kituo cha kupooza umeme kutoka kidatu

 


Waziri wa nishati Dk Medard Kaleman ametoa siku kumi kuanza kwa ujenzi  wa mradi wa kituo cha kupooza umeme kutoka kidatu,ambacho kitasambaza umeme maeneo ya ifakara,mahenge na ulanga MKoani MOrogoro ambapo ujenzi wake unasuasua na kumtaka mkandarasi kujenga mradi huo usiku na mchana huku  akihakikisha   mradi unakamilika kwa wakati.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo dakta Kaleman amesema kuwa mradi huo unagharimu  bilioni 23 fedha ambazo zimetolewa na serikali na kumtaka mkandarasi  kuleta vifaa vya kutosha pamoja na wataalam wa kutosha ili mradi ukamilike kwa wakati. 

Aidha dk Kaleman ameutaka  mradi huo kuwa muarobaini wa tatizo la kukatika kwa umeme maeneo ya ifakara,malinyi na ulanga tatizo ambalo linalalamikiwa na wananchi na kutaka wananchi wapate umeme wa uwakika 

Dk Kaleman pia ameitaka bodi ya wakala wa usambazaji umeme vijijini rea kuweka kambi kwenye mradi huo  na kuanza kazi mara moja huku akiitaka bodi hiyo kutomuongezea muda mkandarasi bali imsimamie mradi ukamilike ndani ya wakati.

Awali akielezea maendeleo ya mradi huo meneja mradi kutoka Tanesco DIDAS LYAMUYA amesema kuwa mbaka sasa mkandarasi yupo kwenye zoezi la ujazaji wa kifusi huku changamoto iliyopo ni tafsiri na kwa namna gani kifusi kijazwe ili samani ya fedha iweze kuonekana.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...