Search This Blog

Monday, February 8, 2021

Watu wasiopungua 10 wauawa kwenye mlipuko wa bomu mjini Mogadishu Somalia

Takriban watu 10 pamoja na mkuu wa ujasusi wameripotiwa kufariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kando ya barabara nchini Somalia.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya eneo hilo, watu wasiopungua 10, pamoja na mkuu wa ujasusi wa eneo hilo, Abdirashid Abdinur Qoje, waliuawa baada ya bomu kulipuka kando ya barabara karibu na eneo la Dhusamareb, mkoani Galmudug.

Maafisa watatu wa polisi walijeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa kwenye barabara ya Mogadishu-Afgoye inayojengwa katika mji mkuu Mogadishu nyakati za asubuhi.

Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...