Search This Blog

Saturday, February 20, 2021

Watu elfu 380 wameyakimbia makazi yao kutokana na mafuriko Indonesia


Watu elfu 380 wameyakimbia makazi yao kutokana na mafuriko yaliyotokea Jakarta, mji mkuu wa Indonesia.

Sabdo Kurnianto, mkuu wa Wakala wa Maafa wa Jakarta, amesema kuwa mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha tangu jana usiku imesababisha mafuriko huko Jakarta Kusini na sehemu za Mashariki.

Kurnianto amesema kuwa watu elfu 380 waliathiriwa vibaya na mafuriko na kwamba juhudi za misaada zinaendelea.

Wakati huo huo, Mamlaka ya Hali ya Hewa, imeonya juu ya mvua kubwa hadi kesho katika miji ya Jakarta, Bogor, Bekasi, Tangerang na Depok.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...