Search This Blog

Tuesday, February 16, 2021

Watu 60 wafa maji baada ya boti kuzama mto Congo


Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema zaidi ya watu 60 wamezama baada ya mashua kupinduka na kuzama katika mto Congo.

Watu 300 wameokolewa lakini inakisiwa kuwa watu wengine 200 hawajilikani walipo baada ya ajali hiyo.

Wakazi wanasema boti iligonga mwamba mashariki mwa mji mkuu Kinshasa, wakati walipokuwa wakisafiri usiku, safari za majini nyakati za usiku zimepigwa marufuku nchini humo.

Waziri wa masuala ya kibinadamu, Steve Mbikayi, ametaka wale wamiliki wa boti kushtakiwa.

"Chombo kilichojaa kupita kiasi, kilichokuwa na abkiria zaidi ya 700 kilipinduka Mai-Ndombe! Miili 60 tayari imepatikana na watu 300 wamenusurika Tunazipa pole familia zilizofiwa na tunataka hatua zichukuliwa dhidi ya wale wote wanaohusika na sekta ya uchukuzi,"aliandika Waziri huyo kwenye mtandao wa Twitter.

Kuna barabara chache nchini DRC na shughuli nyingi za usafiishaji wa mizigo na abiria hufanywa kwa njia ya mto.






No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...