Wakazi wa kijiji cha Kalembela Wilayani Urambo Mkoani Tabora,wameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya Jamii. (TASAF) kwa kuwatatulia kero ya huduma ya Maji safi na salama na kuwatua ndoo wakinamama.
Wakazi hao wametoa shukurani hizo jana wakati wa ziara ya viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) Makao makuu waliongozana na waandishi wa habari kuangalia mafanikio mbalimbali waliopta walengwa wa TASAF kutoka na fedha wanazopata.
Asha Saidi alisema kupitia TASAF waliwapa fursa ya kuchagua mradi moja kati ya utengenezaji wa barabara na maji na ndipo wao waliona maji ni muhimu kuliko mradi mwingine.
Alisema wakazi wa Kijiji hicho walichukua hatua hiyo kutokana na adha ya shida ya maji waliyokuwa wakipata ya kutafuta umbali mrefu ambao ulifikia kilometa tatu kwenye visima vifupi na madimbi ambapo wakati wa kiangazi walikuwa wakipata shida ya kukosa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Mkazi huyo alisema kabla ya mradi wa TASAF walikuwa wakinunua maji kwa gharama ya dumu moja la lita ishirini kwa shilingi mia mbili(200/-) ,baada ya kukamilika kwa mradi huo wamepata nafuu na hivi sasa wananua kwa shilingi 50/= kwa lita hizo.
Aliongeza mradi huo umeleta amani kwa wananchi wote wanaume na wanawake na hivyo kutumia muda walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
Naye Mratibu wa TASAF Wilaya ya Urambo Danford Jacob alisema mpango wa TASAF umesaidia kutekeleza miradi ya visima katika vijiji vinne kwa gharama ya shilingi milioni 256.2.
Alisema vijiji ambavyo vimepata maji kupitia TASAF ni Kalembelea ambapo mradi wao umegharimu kiasi cha milion 67.
Jacob alisema katika mradi huo TASAF imetoa zaidi ya shilingi milioni 63 na nguvu za wananchi ni milion 3.
Alisema gharama hizo zinahusisha ununuzi wa sola 6 ,ujenzi magati mawili na ununuzI wa Tengi la Lita 10,000 na uwekaji mtandao wa vituo vya kuchotea maji.
Jacob alisema mradi huo umewasaidia wananchi 2,270 ambapo wastani wa kupata maji ya uhakika umefikia asilimia 78 kutoka asilimia 34.
Alitaja vijiji vingine vilivyonufaika na TASAF ni Katunguru,Sipungu na Mkola.
Jacob alisema miradi yote imekamilika kwa asilimia miamoja na wananchi wameanza kupata maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment