Shule zimeamrishwa kufungwa isipokuwa madarasa ya watahiniwa kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19.
Mikusanyiko ya watu, ikiwemo ya kidini pia imepigwa marufuku katika sheria mpya za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Makampuni yametolewa wito kuwaruhusu wafanyakazi wanaotoa huduma zisizo za lazima kukaa nyumbani.
Huduma za usafiri wa umma zitaendelea lakini magari yatatakiwa kubeba nusu ya abiria na wasafiri watatakiwa kuvaa barakoa.
Sudan ilikuwa ilikuwa chini ya kipindi cha amri ya kukaa nyumbani hadi mwezi Mei ilipoondolewa wakati wataalamu waliponya kuwa inaweza kusababisha maafa.

No comments:
Post a Comment