Search This Blog

Monday, February 1, 2021

Uturuki yalaani shambulizi la bomu katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu


Uturuki yalaani shambulizi la bomu katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, lililofanyika jana.

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje, ilielezwa kwa masikitiko kwamba watu wengi walipoteza maisha na kujeruhiwa katika shambulizi la bomu jana na shirika la kigaidi la Al Shabab kwenye Hoteli ya Afrika huko Mogadishu, Somalia.

Taarifa hiyo ilisema,

"Tunalaani vikali shambulizi hili baya. Tunatoa pole kwa wananchi wa Somali na serikali nzima kwa ujumla.Tunawaombea rehma za Mungu wale wote waliopoteza maisha na kuwaombea uponaji wa haraka wale wote waliojeruhiwa. Uturuki, itaendelea kusimama na Somalia katika vita dhidi ya ugaidi. "



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...