Muungano wa vyama vya upinzani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati umesema utajitoa kwenye uchaguzi wa bunge, siku moja baada ya mahakama ya katiba kukataa ombi lao la kutaka duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais ibatilishwe.
Muungano huo umesema kwa kutangaza matokeo ya duru ya kwanza licha ya kasoro nyingi zilizojitokeza mahakama ya katiba imethibitisha kuwa uchaguzi huo hauna maana.
Rais aliye madarakani, Faustin Archange Touadera, alichaguliwa tena katika duru ya kwanza ya uchaguzi ambao asilimia 35 tu ya raia walijitokeza kupiga kura.
Taifa hilo limetumbukia katika ghasia tangu mwaka 2013, alipoondolewa madarakani rais Francois Bozize. Serikali ya Touadera inadhibiti thuluthi moja tu ya nchi hiyo.
Thuluthi mbili iliyobakia iko chini ya mikono ya makundi ya waasi, ambayo mara nyingi yanapigania utajiri wa madini uliobarikiwa nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment