Umoja wa Mataifa na wanachama wa Ulaya wa Baraza la Usalama jana Ijumaa waliitaka Israeli isimamishe ubomoaji wa makazi ya Wabedouin katika Bonde la Jordan na kuruhusu kupelekwa kwa msaada wa kibinadamu kwa jamii inayoishi katika eneo la Humsa Al-Baqaia.
Katika taarifa ya pamoja mwishoni mwa kikao cha kila mwezi cha baraza hilo la usalama kuhusu mzozo katika maeneo ya Mashariki ya Kati, Estonia, Ufaransa, Ireland, norway na Uingereza, walisema kuwa wana wasiwasi kuhusu ubomoaji wa mara kwa mara wa hivi karibuni na kutwaliwa kwa bidhaa zinazojumuisha miundo iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya na wafadhili wengine vitendo vinavyofanywa na mamlaka ya Israeli katika eneo la Humsa Al-Bqaia katika bonde la Jordan.
Mjumbe wa UN katika eneo hilo, Tor Wennesland kutoka Norway, pia alielezea wasiwasi wake juu ya ubomoaji na unyakuzi wa ardhi.
Alisema vikosi vya usalama vya Israeli vimebomoa au kutwaa miundo 80 katika jamii ya Bedouinna kwamba vitendo hivyo vimesababisha watu 63 kupoteza makazi ikiwa ni pamoja na watoto 36.

No comments:
Post a Comment