Search This Blog

Sunday, February 7, 2021

Ucjaguzi wa Somalia kucheleweshwa


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amesema uchaguzi wa Somalia, uliotarajiwa kufanyika Februari 8, utacheleweshwa baada ya kuvunjika mazungumzo kati ya viongozi wa kisiasa. 


Rais huyo wa Somalia alieleza hayo bungeni katika mkutano wa dharura na amesema msukosuko huo unaweza kusababisha mzozo wa kisiasa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika inayokabiliwa na machafuko.


 Farmajo, ambaye muda wake unamalizika rasmi katika siku mbili zijazo, atabakia kuwa rais hadi tarehe mpya ya uchaguzi itakapokubaliwa ambapo atawania kuchaguliwa tena kwa miaka mingine minne. Rais wa Somalia na washirika wake wanawalaumu viongozi wa Jubbaland na Puntland kwa kucheleweshwa uchaguzi huo. 


Katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri wa Habari wa Somalia Osman Dubbe alimeyalaumu majimbo hayo mawili kwa kushirikiana na Kenya. Uhusiano wa Somalia na Kenya uilivunjika baada ya Somalia kuishutumu Kenya kwa kuingilia kati mambo yake ya ndani.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...