Search This Blog

Sunday, February 21, 2021

Uchunguzi wa madai ya rais mwezi mmoja mamlakani


Katika kipindi cha wiki nne akiwa katika ikulu ya White House, Rais Joe Biden amekuwa akizungumzia kuhusu changamoto ambazo Marekani inakabiliana nazo kuanzia zile zinazosababishwa na virusi vya corona na uchumi - ambayo yamesababishwa na sera za mtangulizi wake Donald Trump.


Tumeangalia ukweli kuhusu baadhi ya madai ambayo amekuwa akiyatoa


Madai: "Wakati nilipoingia madarakani wiki tatu tu zilizopitanchi hii haikuwa na mpango au chanjo za kutosha"


Rais Biden amekuwa akirejelea mara kwa mara kukosoa utawala uliotanguliwa kwa mpango wake wa chanjo.


Utawala wake ulichapijsha mpango wa chanjo mwezi Septemba mwaka jana uliooelezea mkakati wa kusambaza chanjo katika majimbo nchini humo.


Hatahivyo, kama tulivyoripoti awali, kulikuwa na malalamiko kuhusu jinsi ulikvyotekelezwa, ukosefu wa ufadhili kutoka kwa serikali ya shirikisho jambo ambalo lilisababisha matatizo ya vifaa katika ngazi za mwanzo wakati chanjo zilipofikishwa katika maeneo hayo.


Inapokuja katika suala la iwapo kulikuwa na chanjo za ''kutosha'', utawala wa Trump ulipata dozi milioni 400 kutoka kampuni ya Pfizer-BioNTechna Moderna (chanjo mbili ambazo hadi sasa zimeidhinishwa nchini Marekani ). Dozi zote hizo zinatarajiwa kufikishwa katika maeneo hitajika mwezi Julai.


Hiyo haitoshi kuwachanja watu wote wa Marekani (chanjo zote zinahitaji dozi mbili kwa kila mtu) , lakini inaiwezesha Marekani kuanza mpango wa kutoa chanjo haraka kuliko nchi nyingine nyingi zinazoendelea.


Wakati Trump alipoondoka madarakani mwezi Januari, Marekani ilikuwa imewachanja watu milioni 16-kiwango cha juu zaidi cha ndani cha watu waliochanjwa baada ya Israel, Milki za kiarabu UAE na Uingereza.


Utawala wa Trump pia ulikuwa umeweza kusaini mikataba ya jumla ya dozi milioni 500 kutoka katika makampuni ya Johnson & Johnson, Novavax na AstraZeneca - ambazo bado hajaidhinishwa nchini Marekani, lakini zinaweza kuanza kutumiwa baadae mwaka huu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...