Shirika la Kenya la huduma za wanyamapori (KWS) lilijibu ujumbe wa Twitter uliyowekwa mtandaoni na mhifadhi wa wanyama wa Paula Kahumbu ukisema spishi hiyo adimu ya twiga iko hatarini:
KWS imesema maafisa wa shirika la umeme la Kenya, wataweka vigingi vinginevya umeme.
"Ripoti ya awali inaashiria urefu wa vigingi vya umeme kupitia hifadhi ya Soysambuvi uko chini, kuliko urefu wa twiga," sehemu ya taarifa ilisema.
Bi Kahumbu alisema vifo vya wanyama hao vingezuiliwa ikiwa ushauri wa wataalamu ungezingatiwa.

No comments:
Post a Comment