Inter Miami inataka kuwasajili wachezaji wawili wa zamani wa timu ya taifa ya England Ryan Shawcross, 33, kutoka Stoke City na beki Kieran Gibbs, 31, wa West Brom (Sun)
Manchester City watamaliza ushawishi wao kwa mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez wakati mchezaji huyo mwenye miaka 23 anatarajia kusaini mkataba mpya na timu hiyo ya ligi Kuu Serie A
Manchester United watasubiri mpaka mwishoni mwa msimu kabla ya kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na kocha Ole Gunnar Solskjaer, ambaye mkataba wake utakwisha mwishoni mwa 2021-22. (Sun)
Real Madrid wanapendelea kumsajili mlinzi wa kushoto wa Bayern Munich David Alaba, 28, huku Chelsea ikionesha kutokuwa tayari kutimiza takwa la mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki. (ESPN)
AC Milan wanajiandaa kuanza mazungumzo na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 39, kuhusu mkataba mpya ambao utamfanya kuwa na klabu hiyo mpaka atakapofikisha miaka 41. (Sun)
Manchester City itaanza mazungumzo na John Stones 26, kuhusu mkataba msimu huu kwa kutambua jukumu la mlinzi huyo wa England.(Times, subscription required)
Crystal Palace hawajui iwapo watampa kocha Roy Hodgson, 73, mkataba mpya msimu ujao. Mkataba wa sasa unamalizika katika msimu wa joto. (Mail)
Mshambuliaji wa Kiingereza wa Newcastle United Dwight Gayle, 31, amefadhaishwa na kutopangwa kucheza katika uwanja wa St James 'Park na anaweza kuondoka kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake ukimalizika msimu wa joto. (Chronicle)
Mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen, 31, anataka kubadilisha uhamisho wake wa mkopo kutoka Roma kwenda Everton kuwa mkataba wa kudumu. (Goal)

No comments:
Post a Comment