Search This Blog

Sunday, February 7, 2021

Tetesi za soka kimataifa

 


Kocha wa Tottenham Jose Mourinho anaamini kuwa ni jambo la kusubiri ''muda unaofaa'' linapokuja suala la mazungumzo kuhusu mkataba mpya kwa ajili ya mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, ambaye mkataba wake na Spurs utakwisha mwaka 2023. (Evening Standard)

Kujeruhiwa kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mhispania Sergio Ramos kunaweza kusimamisha mazungumzo yake kuhusu mkataba mpya na Real Madrid mpaka atakapopona, makataba wa mchezaji huyo mwenye miaka 34 unamalizika majira ya joto. (Marca)

Kocha wa AC Milan Stefano Pioli amesema ni ''sawa'' kwa mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovich ''kuendelea kucheza'' katika klabu hiyo ya Italia. Mkataba wa mchezaji huyo, 39 na klabu hiyo ya Serie A unakamilika msimu wa joto (Sky Sports Italia, via Football Italia)

Mkurugenzi wa mpira wa miguu wa Ajax Marc Overmars anajiandaa kuondoka kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa msimu, huku winga huyo wa zamani wa Uholanzi akihusishwa na taarifa za kujiunga na Barcelona au Arsenal. (Mundo Deportivo)

Kiungo wa kati Mfaransa Tanguy Ndombele, 24, amekubali kuwa ilibidi abadilike kama alitaka kufanikiwa akiwa na Tottenham katika ligi ya Primia.(Telegraph - subscription required)

Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson anatarajia winga Wilfried Zaha atapenda kuwa na kikosi hicho, mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Ivory Coast ana malengo ya kucheza Ligi ya Mabingwa. (Mail)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 24, hajafunga katika michezo ya ligi ya Primia lakini amesema, pamoja na kwamba hajafunga kwa ''muda mrefu'' ataendelea kucheza na ''magoli yatakuja''. (Evening Standard)

Mwamuzi wa zamani wa Ligi Kuu ya England Mark Halsey amesema VAR inaonekana kama ''kichekesho'' lakini ''tunapaswa kuwafikiria waamuzi, ambao wanakaribia kuchoka''. (Sun)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...