Search This Blog

Monday, February 15, 2021

Tetesi za soka kimatafa


Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos atagharimu Arsenal pauni milioni 22 zikiwa zinataka kumnunua moja kwa moja Real Madrid msimu huu. (Mirror)

Arsenal inaonekana kuwa karibu kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting Lisbon, 18, raia wa Ureno Tiago Tomas msimu huu. (Sun)

Arsenal imearifiwa kuwa inaweza kumsajili mshambuliaji wa Celtic Odsonne Edouard, 23, kwa pauni milioni 15m. (Express)

Liverpool na Manchester City zinamnyatia kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Florian Neuhaus, 23. (Kicker)

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anamuwinda aliyekuwa mlinda lango wake Tottenham Hugo Lloris. (Football Insider)

Mlinzi wa Brazil David Luiz, 33, anatarajiwa kusaini makubaliano mapya ya kuendeleza mkataba wake Arsenal. (Independent)

Celtic inafuatilia kwa karibu uhamisho wa kiungo wa kati wa Burnley na Jamhuri ya Ireland Robbie Brady, 29. (Mirror)

Burnley inafikiria kumsajili mlinda lango wa Benfica raia wa Marekani Carlos Joaquim dos Santos, 20. (Sun)

Bayern Munich inaimarisha juhudi zake za kumsaka beki wa kulia wa Norwich City Max Aarons, 21. (Mail)

Newcastle imepewa fursa ya kumsaili aliyekuwa mchezaji wa Liverpool na Chelsea mshambuliaji Daniel Sturridge. Mchezaji huyo, 31, amekuwa bila klabu tangu alipoondoka Trabzonspor. (90Min)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea na Atletico Madrid Diego Costa yuko katika mazungumzo ya kujiunga na klabu yake akiwa kijana ya Palmeiras. Mkataba wa Costa, 32, ulikatishwa na Atletico mnamo mwezi Januari. (Sky Sports)

Mlinzi wa Sevilla, Mfaransa Jules Kounde, 22, ameibuka kuwa mchezaji wa juu anayelengwa na Manchester United

Mlinzi wa Sevilla , Mfaransa Jules Kounde,22, ameibuka kuwa mchezaji wa juu anayelengwa na Manchester United baada ya Bayern Munich kumnyakua beki wa kati Dayot Upamecano, 22, kutoka RB Leipzig. (Express)

Liverpool, Manchester City, Juventus na Bayern Munich wanamfuatilia kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Florian Neuhaus, 23. (90 min)

Ole Gunnar Solskjaer amekiri kuwa anamfuatilia mshambuliaji wa Borrusia Dortumund Erling Braut Haaland

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer amekiri kuwa anamfuatilia mshambuliaji wa Borrusia Dortumund Erling Braut Haaland, 20 baada ya kushindwa kumsajili mwaka jana. (MEN)

Real Madrid wanamfuatilia Aymeric Laporte wa Manchester City na wanaweza kujaribu kumsajili mlinzi huyo wa kifaransa, 26, majira ya joto. (Star)

Arsenal hawajapoteza matumaini ya kuridhia mkataba mpya na mshambuliaji wa Kiingereza Folarin Balogun, 19. (Sun)

Winga wa Morocco na klabu ya Chelsea Hakim Ziyech, 27, anafikiria kuhusu mustakabali wake ndani ya klabu baada ya kutafuta nafasi ya kucheza tangu alipojiunga akitokea Ajax. (Corriere Dello Sport-in Italian)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...