Search This Blog

Sunday, February 28, 2021

TAKUKURU yawafikisha mahakamani wanafunzi wawili wa Chuo cha Mipango Dodoma kwa Rushwa

 


Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma leo imewapandisha kizimbani watu watu katika mahakama ya Hakimu mkazi Dodoma kwa makosa mbalimbali ya kushawishi na kupokea rushwa kinyume na taratibu.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo imewataja watuhumiwa waliopandishwa kizimbani miongoni mwao ni aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma Bw. Patrick Abohokile (26) kwa kosa la kushawishi ili apokea kiasi cha shilingi 340,000 na kufanikiwa kupokea 320,000.


“TAKUKURU imempandisha kizimbani Patrick Abohokile tunamfungulia mashtaka manne moja kwa kushawishi ili kupokea 340,000 na kufanikiwa kupokea 320,000 kutoka wanafunzi wawili wa mwaka wa tatu wa chuo hicho waliokuwa wamefanya mitihani wa marudio wa somo la Appplied Statics II ili awasaidie kurudia mtihani huo nje ya mfumo rasmi wa chuo” Amesema.


Katika shauri la pili Rufus Msemwa (32) amefungiliwa mashtaka mawili ya kuahidi kutoa rushwa ya shilingi elfu 20,000 kwa mwanafunzi mwenzake ili asaidiwe kurudia mtihani wa somo la Applied Statics II nje ya mfumo rasmi wa mfumo wa chuo.


Bw. Kibwengo amesema katika uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa Novemba 2, 2020 washtakiwa wakishirikiana na watu wengine ambao bado wanatafutwa ambao walisaidia kuwawezesha baadhi ya wanafunzi kufanya mtihani wa IRDP nje ya mfumo wa chuo.


Aidha katika hatua nyingine wanatarajia kumfikisha katika Mahakama hiyo Mtendaji wa Kijiji cha Chanugulu Wilaya ya Chamwino Bw. Peter Kyara (36) kwa kosa la kushawishi rushwa ya shilingi laki tano(500,000) kwa mwananchi mmoja ili asishitakiwe kwa kosa la mifugo yake kuingia katika shamba la mkulima.


“Uchunguzi wa TAKUKURU umeonyesha  kwamba tarehe 10, Disemba 2020 mshtakiwa alimtaka mwananchi mmoja ampe hongo ili asimchukulie hatua baada ya kushtakiwa kwake kwa kosa la kuchunga mifugo kwenye shamba la mwananchi mmoja” amesema.


Ameongeza kuwa “ tunawaasa vijana wa Mkoa wa Dodoma kujiepusha na njia za mkato na kuwataka wajibidishe katika masomo na kila jambo wanalolifanya, pia tunawakumbusha watendaji katika kata, mitaa na vijiji kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuzingatia taratibu” amesema.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...