Search This Blog

Sunday, February 21, 2021

Somalia yaikosoa UAE kwa kauli yao dhidi ya serikali


Serikali ya Somalia imekosoa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuiita "serikali ya mpito", ikimaanisha utawala wa Mogadishu kufuatia ghasia za Mogadishu za Ijumaa.

Waziri wa Habari wa Somalia Osman Abukar Dubbe alisema kuwa tathmini ya UAE juu ya utawala wa Mogadishu na kuiita "serikali ya mpito" ni mpango wa kudhoofisha Somalia.

Dubbe aliongezea kusema kuwa serikali ya Somalia haitambui taarifa ya UAE kuhusu matukio yanayofanyika nchini humo.

Akiashiria kwamba UAE inataka Somalia iwe kama Libya na Yemen, Dubbe alisema,

"Hili ni jambo ambalo watu wa Somalia wanafahamu."

Dubbe alibaini kuwa baada ya makubaliano ya Septemba 17 kutiwa saini, viongozi wengine wa serikali walikwenda UAE kukutana na maafisa, na kisha wakaingilia kati makubaliano ya uchaguzi.

Waziri Dubbe aliitaka UAE iombe radhi kwa kukiuka uhuru wa Somalia na kuita Serikali ya kuu ya Somalia (TFG) "serikali ya mpito".



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...