Search This Blog

Friday, February 12, 2021

Simba yaweka heshima, yaitandika AS Vita 1-0


 CRIS Mugalu, mshambuliaji wa kikosi cha Simba, usiku wa kuamkia leo amepeleka shangwe kwa Watanzania kwa kufunga bao la ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi. 

Ikiwa Congo, Simba chini ya Didier Gomes ilicheza kwa kujilinda huku ikishambulia kwa kushtukiza kwa lango la AS Vita inayonolewa na Frolent Ibenge ambaye anainoa pia timu ya Taifa ya Congo.


Bao pekee la ushindi kwa Simba lilipachikwa dakika ya 60 kwa mkwaju wa penalti uliolindwa mpaka dakika 90 na kuifanya timu hiyo kubeba pointi tatu ugenini.


Ni kiungo Luis Miquissone ambaye alisababisha penalti hiyo baada ya kupiga mpira uliokutana na mikono ya mchezaji wa AS Vita kwa pasi ya Clatous Chama.


Mchezo ulichezwa Uwanja wa De Martyrs ambapo wenyeji walianza kwa kushambulia kwa kasi huku Simba wakilazimisha kujilinda na kushambilia kwa kushtukiza.


Bado Gomes ana kazi kwa upande wa kuweka sawa safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikifanya makosa ya mara kwa mara yalikuwa yakimlazimu Aishi Manula kukosa utulivu ndani ya lango kwa muda wote wa dakika 90.


Uimara wake pia ndani ya lango umeweza kuifanya Simba kuwa kwenye mikono salama na kusepa na pointi tatu muhimu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


Gomes amesema kuwa anawapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa juhudi na kutimiza majukumu ambayo aliwapa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...