Rais Erdoğan alishiriki infographic kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii na kuzungumzia maendeleo yaliyopatikana katika elimu ya juu wakati wa utawala wake.
Idadi ya vyuo vikuu iliongezeka kutoka 76 mwaka 2002 hadi 207 mwaka 2021. Bajeti ya elimu ya juu ilipanda kutoka lira bilioni 2.5 hadi lira bilioni 36.
Wakati idadi ya wanafunzi ikionekana kuwa milioni 1 na laki 6 mnamo mwaka 2002, idadi hii imefikia milioni 8 na laki 4 kwa sasa.
Idadi ya wahadhiri iliongezeka kutoka elfu 70 hadi laki 1 na elfu 80. Sehemu ya wasomi wa kike katika mfumo wa elimu ya juu ilikuwa takriban alama 5 juu ya wastani wa asilimia 40 katika Jumuiya ya Ulaya.
Idadi ya wanafunzi wa kike, ambayo ilikuwa asilimia 42 hapo awali, imeongezeka hadi asilimia 49 mwaka huu.
Zaidi ya wanafunzi laki 2 kutoka kote ulimwenguni wanajiandaa kwa siku zijazo katika vyuo vikuu vya Kituruki.
Uturuki, ilikuwa ya kwanza kupokea maombi ya usajili wa vyuo vikuu barani Ulaya.
Kulingana na data kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Uturuki iliorodheshwa katika nchi 10 bora duniani kwa mafanikio yake ya idadi kubwa ya wanafunzi wa kimataifa.
Rais Erdoğan alisema,
"Juhudi zetu za kuboresha elimu ya juu ni mchakato usio na mwisho. Sisi, kama ofisi ya Urais, tumepanga njia zetu zote kwa vijana wetu kupata elimu yenye sifa."

No comments:
Post a Comment