Rais wa Afrika Kusini ,Cyril Ramaphosa ameelezea wadhifa wake kama Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika(AU) kuwa sawa na "kubatizwa kwa moto".
Muhula wake wa mwaka mmoja kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika utamalizika baada ya wiki hii na kiti hicho kitachukuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo Félix Tshisekedi.
Bw Ramaphosa amesema kazi yake kubwa katika kipindi cha mwaka mzima uliopita ilikuwa ni kuliongoza bara wakati wa kipindi cha janga la dunia la corona.
Ametaja mafanikio mengine katika upande wa kuimarisha Amani, kuwawezesha wanawake kufungua biashara katika bara la Afrika.
"Katika kipindi hicho, eneo huru la biashara (AfCFTA) liliweza kuzinduliwa na kutangazwa kwa ari mpya ya biashara baina ya mataifa ya Afrika na ushirikiano wa kiuchumi," aliandika.
No comments:
Post a Comment