Search This Blog

Monday, February 1, 2021

Nigeria kuisaidia Msumbiji kukabiliana na ugaidi


Nigeria imesema iko tayari kushirikisha ujuzi wake wa mapambano dhidi ya wanamgambo wa KiislamuImage caption: Nigeria imesema iko tayari kushirikisha ujuzi wake wa mapambano dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu

Nigeria imejitolea kuisaidia Msumbiji katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu katika jimbo lenye utajiri wa mafuta llililopo kaskazini mwa Msumbiji, mji wa Cabo Delgado.

Zaidi ya watu 2,000 wameuawa na wengine zaidi ya 500,000 wamekimbia ghasia, kwa mujibu wa kamati ya Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.

Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria , Geoffrey Onyeama, alitembelea Msumbiji mwishoni mwa juma na kukutana na Waziri Mkuu Carlos Agostinho do Rosário.

Bw Onyeama alisema kuwa Nigeria iko tayari kushirikisha uzoefu wake wa kupambana wanamgambo wa Kiislamu na kutoa usaidizi kwa Msumbiji.

Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya ziara ya kidiplomasia aliyoifanyika katika nchi za kusini mwa Afrika kuhamasisha uungaji mkono nia ya Nigeria kuwa mwenyekiti wa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika.

Tanzania, Afrika Kusini na Burkinafaso pia zinawania kiti hicho,

Uchaguzi utafanyika wakati wa kikao cha AU kilichopangwa kufanyika wiki hii.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...