Jopo la wataalamu wa kimataifa ambao wanachunguza chanzo cha Covid-19 limeitupilia mbali nadharia kuwa virusi vya Corona vilitengenezwa maabara.
Peter Ben Embarek, mkuu wa jopo la wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) , alisema ilikuwa ni vigumu mno kuhusisha virusi na maabara ya China iliyopo mji wa Wuhan.
Alisema kazi zaidi inahitajika kufanyika ili kubaini chanzo cha virusi hivyo.
Maoni hayo yalitolewa wakati wa kuhitimisha kazi ambayo WHO waliokuwa wameenda kuifanya pamoja na China.
Wuhan, ambayo ipo jimbo la Hubei Magharibi mwa China , ni eneo la kwanza duniani kugundulika kuwa na virusi hivyo vya corona.
Tangu wakati huo zaidi ya kesi milioni 106 zimeripotiwa na vifo milioni 2.3 vimeripotiwa duniani kote.
Dkt Embarek amewaambia waandishi wa habari kuwa uchunguzi haujaweza kupata taarifa mpya ambayo inaweza kubadili picha ya mlipuko wa corona.
Wataalamu wanaamini virusi hivyo vilianzia kwa wanyama kabla ya kusambaa kwa binadamu, lakini hawana uhakika ilikuaje.
Dkt. Embarek alisema kazi ya kubaini chanzo cha Covid-19 kinatajwa kuwa kilianzia kwenye popo, lakini hawana uhakika kama jambo hilo lilitokea Wuhan.
Alisema kugundua namna ambavyo mnyama alisababisha maambukizi hiyo ni kazi nyingine inayoendelea kufanyiwa kazi, lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa ilitoka kwa vilitoka kwa mnyama na kwenda kwa binadamu.
Wataalamu wamesema pia hakuna viashiria vinavyoeleza jinsi virusi vilivyosambaa Wuhan kabla ya kesi ya kwanza kurekodiwa mwezi Desemba 2019.
Liang Wannian, ni mtaalamu wa tume ya afya nchini China, amesema Covid-19 inawezekana hata ilianza katika eneo lingine kabla haijagundulika Wuhan.
Timu hiyo inataka kufanya uchunguzi zaidi katika vyakula baridi, usafirishaji na biashara ya vyakula vaya baridi.
WHO ilianza uchunguzi huo mwezi uliopita baada ya kukubaliana na China.

No comments:
Post a Comment