Ndege ambaye ameonekana kuwa nusu-jike na nusu-dume amepigwa picha jimboni Pennsylvania na mfuatiliaji ndege baada ya kumsikia rafiki yake ambaye alimuona ndege huyo.
Ndege wa namna hii mwenye maumbile mchanganyiko ni nadra kuonekana.
Ndege aina ya cardinals dume ni wekundu lakini jike huwa ni rangi ya udongo iliyofifia, ikimaanisha kuwa spishi za ndege huyu pengine ni mchanganyiko wa jinsia mbili.
Mtaalamu wa masuala ya ndege Jamie Hill, 69, ameiambia BBC kuwa ilikuwa ni ''mara moja katika maisha, mara moja kati ya milioni''. Kukutana na ndege huyo.
Rafiki wa Bwana Hill alimwambia amemuona ''ndege asiye wa kawaida'' akifika katika malisho ya ndege katika kaunti ya Warren huko Pennsylvania.
Mara ya kwanza Bwana Hill alijiuliza ikiwa ndege huyo alikuwa na athari ya melanini kwenye manyoya yake, lakini hatakuwa nusu-jike, nusu-dume.
Lakini baada ya kuona picha kwenye simu, alishuku kuwa ndege huyo alikuwa na jinsia mbili, maana yake akiwa na ovari inayofanya kazi na korodani inayofanya kazi.
Ndani ya saa moja aliweza kumpiga picha ndege huyo wa ajabu.
''Baada ya kupata picha, moyo wangu ulikuwa unadunda kwa saa tano mpaka nilipowasili nyumbani na kuzitengeneza picha ili kuona kile nilichonacho,'' alisema Bw.Hill.

No comments:
Post a Comment