Search This Blog

Wednesday, February 24, 2021

Ndege Maalum yaanza kuwadhibiti Nzige waliovamia Simanjiro


 Na John Walter-Manyara

Baada ya kundi Nzige kuvamia wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Mkuu wa wilaya hiyo Zephania Chaula, amesema Wataalamu wanaendelea na shughuli ya kuwadhibiti Nzige hao ili wasifanye uharibifu.

"Mpaka sasa hawajaleta madhara yoyote kwenye mazao kwa sababu hawajatua kwenye mashamba, wamekuwa wakitua kwenye maeneo yenye malisho, kwa hiyo athari inaweza ikawa kwenye upande wa mifugo katika maeneo yao malisho ila naamini watadhibitiwa shida haitokuwepo" alisema Chaula

Chaula akizungumza na Smile Fm redio iliopo makao makuu ya Mkoa wa Manyara mjini Babati, amesema kwa kutumia ndege maalum inayotumika kuwaua Nzige hao, ana amini wataalamu wa kilimo katika wilaya yake na kutoka wizara ya Kilimo wataweza kuwadhibiti wadudu hao waharibifu wa Mazao na Majani.

Amewataka wananchi wa Simanjiro kuwa watulivu wakati serikali inashughulika na suala hilo kwa kuwa ana imani kubwa na waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda na Naibu wake Hussein Bashe kwa kazi ya uhakika wanayoifanya.

Amewatoa hofu wananchi kwa kuwaambia kuwa katika wilaya ya Simanjiro hakuna njaa, Chakula kitaendelea kuwepo kwa kuwa mvua zinanyesha na wananchi wanalima huku akiwasisitiza kulima kilimo cha Kisasa.

Kwa upande mwingine amesisitiza kuwa wilaya yake na Viunga vyake vyote hali ya ulinzi na usalama ipo vizuri wakati wote.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...