Search This Blog

Tuesday, February 16, 2021

Muhimbili watoa ufafanuzi baada ya vitanda kuonekana nje


Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa huwa inao utaratibu wa kupuliza dawa ya kuuwa wadudu karibu maeneo yote ya hospitali na kwamba wakati wa zoezi hilo wagonjwa hutolewa nje na kuwekwa chini ya mahema.

Kauli hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa hospitali hiyo, baada ya picha kusambaa mitandaoni zikionesha vitanda vya hospitali hiyo vikiwa vimetolewa nje na kuwekwa kwenye mahema.

“Hospitali ina kawaida ya kupuliza dawa ya kuua wadudu mbalimbali wodini, maofisini na maeneo mengine ya nje mara mbili kwa mwaka, wakati zoezi likifanyika, wagonjwa  hutolewa nje na kuwekwa chini ya mahema huku huduma nyingine zikiendelea, hili ni zoezi la kawaida na endelevu”, imeeleza taarifa hiyo



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...