Search This Blog

Friday, February 19, 2021

Msiwafumbie macho wanafunzi wanao kiuka maadilii


Na Farida  Saidy, Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewataka wajumbe wa Bodi za Shule za Sekondari Mkoani hapa kutowafumbia macho Wanafunzi wote wanaokiuka taratibu na maadili ya Shuleni,kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza nidhamu baina ya Wanafunzi na waalimu na kuongeza ufaulu.

Loata Sanare ameyasema hayo February 19 alipokuwa anapokea Madawati na viti 110 kutoka  Benki ya NMB,ambao amesema Serikali  ya awamu ya tano pamoja na wazazi wanahangaika kwa ajili ya watoto wao wapate elimu,hivyo si vyema kwa Wanafunzi kuacha masomo na kujihusisha na masuala yasio na madili

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo ametoa pongezi kwa NMB  kanda ya Mashariki kwa kuwa na Utamaduni wa kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo  hususan katika sekta ya elimu

Naye Diwani wa Kata ya Kilakala Marco Kanga amewataka walimu na menejimenti za Shule zilizopata msaada  wa viti na Madawati kutunza miundombinu hiyo ili iwasaidie kwa muda mrefu.

Shule zilizopokea msaada huo ni Shule ya Sekondari ya Lupangailiyoko Kata ya Kilakala na Shule ya Sekondari ya Kihonda Kata ya Mazimbu



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...