Search This Blog

Wednesday, February 3, 2021

Mshirika wake Rais Tshisekedi ateuliwa kuwa spika mpya


Christophe Mboso N'Kodia Pwanga mwenye umri wa miaka 78 ndiye Spika mpya wa Bunge, nchini DRC.

Wadhifa huo ameupata baada ya kupata wingi wa kura kutoka kwa wabunge katika uchaguzi uliofanyika jana Jumatano na hivyo kuchukua nafasi ya spika wa zamani, Jeanine Mabunda aliyeondolewa, mapema mwezi Desemba kwa madai ya ubadhilifu wa fedha za Bunge.

Spika mpya atajiunga na wabunge 391 kuunda serikali mpya ya Rais wa sasa wa DRC, Felix Tshisekedi.

Uchaguzi wa spika huyo mpya unadaiwa kuwa ishara mpya kuwa siasa za DRC zinaweza kubadilika na matakwa ya raia kuafikiwa.

Huenda isiwe rahisi kwa Tschisekedi kufanya mageuzi ya kisiasa kutokana na ushawishi wa kisiasa wa mtangulizi wake Joseph Kabila

Lakini kutokana na idadi kubwa ya wabunge kutoka chama chake, alibaki kuwa na nguvu kubwa katika taifa hilo na kuweza kusimamia wizara nyingi muhimu.

Tshisekedi amekuwa akiwatimua washirika wa mtangulizi wake tangu alipovunja muungano mwezi Disemba mwaka jana kufuatia kuongezeka kwa tofauti kuhusiana na mageuzi ya usalama, mahakama, tume ya uchaguzi na mashirika mbalimbali ya taifa.

Rais Tshisekedi - kwa sasa amefanikiwa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na Kabila - hivyo anatarajiwa kuwa ataweza kufanikiwa kufanya mabadiliko na kutimiza ahadi zake ikiwa ni pamoja na kumaliza ghasia katika maeneo ya madini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...