Search This Blog

Friday, February 12, 2021

Mkuu wa zamani wa ECB Draghi kuwa waziri mkuu wa Italia


Rais wa zamani wa Benki Kuu ya Ulaya ECB, Mario Draghi amekubali jukumu la kuwa waziri mkuu mpya wa Italia. 

Draghi mwenye umri wa miaka 73, alijitokeza mbele ya vyombo vya habari baada ya tangazo lililotolewa na msemaji wa kasri la rais, na kutangaza baraza lake la mawaziri, linaloundwa na wanasiasa na watalaamu. 

Awali, Draghi alifanya mashauriano mapana na wawakilishi wa vyama mjini Rome, na alipata uungwaji mkono wa kushangaza kutoka muungano wa shoto ulioshindwa wa mtangulizi wake Giuseppe Conte, pamoja na upinzani. 

Mzozo wa serikali nchini Italia, katikati mwa janga la virusi vya corona, umeendelea tangu katikati mwa mwezi Januari.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...