Search This Blog

Wednesday, February 17, 2021

Mkurugenzi Mkuu mpya wa WTO aonya kuhusu ubaguzi katika usambazaji wa chanjo


Ngozi Okonjo-Iweala, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), ameonya dhidi ya "ubaguzi" katika usambazaji wa chanjo dhidi ya corona.

Okonjo-Iweala ambaye hapo awali alikuwa Kiongozi wa Chama cha Chanjo Duniani (GAVI)

ameiambia BBC, 

"Wakati nchi tajiri zikiwapatia chanjo raia wao, nchi masikini hazipaswi kusubiri chanjo." 

Okonjo-Iweala amesema kuwa katika wiki za hivi karibuni, nchi nyingi zimekuwa zikijaribu kuzuia usafirishaji wa chanjo zinazotengenezwa ndani ya mipaka yao, na kubainisha kuwa hali hii itazuia ahueni ya ulimwengu. 

"Hakuna nchi inayoweza kujisikia salama ikiwa kila nchi itafikiria watu wake.", alisema.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres pia amezitaka nchi zote kuwa na 'mshikamano' na kuondoa 'utaifa wa chanjo' kwa kuunga mkono chanjo kwa watu wote.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...