Search This Blog

Wednesday, February 17, 2021

Mfanyabiashara wa Nigeria ahukumiwa Marekani kwa wizi wa mtandao


Mahakama ya Marekani imemhukumu kifungo cha miaka 10 gerezani mfanyabiashara kwa Kinigeria kwa kuendesha mtandao wa wizi wa mtandaoni na kuiba kiasi cha takribano pauni milioni 8.

Obinwanna Okeke, kwa jina jingine Invictus Obi, alitumia makampuni yenye makazi nchini Nigeria kuwadanganya watu katika jimbo la Virginia nchini Marekani.

Kampuni zake za 'Invictus Group companies' zilitumia barua pepe ili kupata taarifa za kuingia kwenye akaunti za watu kisha kuchukua fedha zao 2015 na mwaka 2019.

Obinwanna- ambaye aliwahi kuwa kwenye orodha ya forbes ya Wafanyabiashara wenye ushawishi wenye umri wa miaka 30- alikamatwa mwezi Agosti mwaka 2019.






No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...