Mfanyabiashara maafuru,Lukas Sotel (50) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Remagwa wilayani Tarime mkoani Mara amerudishwa rumande baada ya kesi yake yamauaji kupigwa kalenda.
Awali mahakama hiyo iliambiwa kuwa mnamo tarehe 09,10, mwaka 2014 katika kijiji cha Buriba wilayani Tarime mkoani Mara mtuhumiwa Sotel alikiuka sheria za Mwenyezi Mungu amri ya sita ikiwemo ile ya Nchi inayokataza kuua na kutenda kosa hilo kinyume cha sheria.
Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi,Isepkta,Salum Athumani aliiambia mahakama ya wilaya kuwa upepelezi wa mtuhumiwa bado haujakamilika na kesi hiyo kupigwa kalenda hadi itakapotajwa tena Tarehe 19,Februal mwaka 2021 ambapo mtuhumiwa alirudishwa Rumande.
Mwendesha mashitaka akimsomea mtuhumiwa kwa mara ya kwanza shitaka hilo linali mkabili mahakamani hapo alisema kuwa mtuhumiwa anatuhumiwa kumuua Wamkuru Nyamohanga ambaye ni mkazi wa kijiji cha Remagwe wilayani hapa kwa kumpiga risasi.
Mtuhumiwa baada ya kusomewa shitaka linalo mkabili alikana mahakamani hapo kuwa hajatenda kosa hilo ambapo alipelekwa kolokoloni ili kusubiri upelelezi utakapo kamilika.
Kesi hiyo ipo chini yahakimi mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Tarime mkoani Mara,Veronica Mugendi.

No comments:
Post a Comment